Siku kama ya leo Smith alimchapa kofi Chris Rock

Siku kama ya leo Smith alimchapa kofi Chris Rock

Tarehe na mwezi kama wa leo miaka miwili iliyopita dunia ilishuhudia kile kilichoitwa utovu wa nidhamu baada ya mwigizaji Will Smith kumchapa kofi mchekeshaji ambaye pia ni mwigizaji Chris Rock mbele ya hadhara katika usiku wa Tuzo za Oscar mwaka 2022.

Kichapo hicho kilikuja baada ya Chris kumtani aliyekuwa mke wa Will, Jada Smith kuhusiana na kichwa chake kutoota nywele, jambo ambalo Smith hakufurahishwa nalo kutokana na kuwa na ugonjwa ambao unasababisha asiote nywele.

Aliyekuwa mke wa Will Smith, Jada anasumbuliwa na ugonjwa uitwao ‘Alopecia Areata’, ambao hauna tiba husababishwa na mfumo wa kinga kushambulia follicles ya nywele na kupelekea mtu kutokuota nywele.

Ikumbukwe kuwa Oktoba mwaka jana #JadaSmith alishika vichwa vya habari baada ya kudai kuwa yeye na #WillSmith walitengana miaka 7 iliyopita licha ya kuwa wanaishi pamoja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags