Shule zafungwa kutokana na kuongezeka kwa kipindupindu, Malawi

Shule zafungwa kutokana na kuongezeka kwa kipindupindu, Malawi

Shule katika miji miwili mikubwa nchini Malawi zitasalia kufungwa hadi wakati usiojulikana kutokana na mripuko wa kipindupindu unaoendelea kuwa mbaya zaidi.

Wanafunzi walitarajiwa kurudi shuleni jana baada ya mapumziko, Lakini wizara ya afya imesema kuanza kwa mihula kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika mji mkuu Lilongwe na mji wa kusini Blantyre kutacheleweshwa kwa angalau wiki mbili.

Waziri wa Afya Khumbize Chiponda amesema kuwa kuahirishwa huko kumetokana na kuongezeka kwa idadi ya visa vya kipindupindu na vifo kuzidi kuongezeka.

Aidha nchi hiyo ya kusini mwa Afrika imerekodi takriban visa 18,000 vya ugonjwa huyo na vifo 595 tangu Machi mwaka jana katika kile Umoja wa Mataifa unasema ni mripuko mkubwa kabisa kuwahi kulikumba taifa hilo katika miaka kumi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags