Shule yafungwa baada ya wanafunzi kufariki

Shule yafungwa baada ya wanafunzi kufariki

Na Asha Charles

Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mukumu nchini Kenya imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi wawili kufariki dunia na wengine takribani 500 kuugua kutokana na kula chakula na kunywa maji yasiyokuwa salama.

Siku za hivi karibuni, Shule hiyo imezua taharuki baada ya idadi kubwa ya wanafunzi kulazwa Hospitali kwa kutapika, kuhara na kizunguzungu huku Maafisa wa Afya nchini humo wakidai kuwa ni kipindupindu.

Aidha Kamati iliyochunguza tukio hilo iligundua nafaka zinazotumiwa Shuleni hapo zinahifadhiwa na kemikali aina ya ‘nova’ zinazodaiwa kuwa na viambata vyenye sumu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags