SHUFAA NASSOR: Mhitimu aliyeamua kuwa muhamasishaji wa hedhi salama

SHUFAA NASSOR: Mhitimu aliyeamua kuwa muhamasishaji wa hedhi salama

Haya haya wanangu sana. I hope mko good wafuatiliaji wa segment yetu ya UniCorner. Leo tumekuja na kitu kipya kabisa yaani sio kila siku tuwe na mada tu.

Katika makala za nyuma zilizopita nilielekeza kuhusiana na kufanya mambo kabla ya kumaliza chuo nilikuwa namaanisha, naamini mkija kusoma hii makala ya huyu mwanadada basi utapigilia mstari kile nilichokieleza hapo awali.

Ukiachana na kile nilichokizungumza kuhusu maisha baada ya kumaliza chuo, sio lazima ufanikiwe kwa kile ambacho umekisomea, wengine hufanikiwa kwa njia nyingine kabisa na sio kila njia aliotumia mwenzio kufanikiwa basi na wewe itakufanya ufanikiwe.

Leo nakusogezea mwanadada ambaye yeye amemaliza chuo na hajapata kazi lakini anaendelea kupambana na maisha yake kwa kuwa muhamasishaji wa hedhi salama.

Shufaa Hemed Nassor ni mwanafunzi aliyemaliza chuo cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS), astashahada ya uuguzi "DIPLOMA IN NURSING," mwaka 2022.

Kufuatiwa na changamoto ambazo amekumbana nazo kipindi cha ukuwaji wake (balehe) ikamuumiza na kumfanya awe mmoja wa kuwasaidia mabinti wenzake wasipitie changamoto alizozipitia yeye.

“Kutokana na baadhi ya changamoto za hedhi nilizowahi pitia nikiwa mdogo na baada ya kupata elimu, niliamua kuanza harakati za masuala ya hedhi salama mwaka 2020, nikiwa mwaka wa kwanza chuoni.” amesema Bi Shufaa.

Hata ya baada ya kumaliza chuo aliendelea na harakati za kutoa elimu kuhusu masuala ya hedhi salama hususani kwa jamii ya watu wanaovaa hijab kama yeye. Kwasababu wengi hao hawana uwezo wa kununua pads nk.

Hedhi salama imefanikiwa kwa kiasi chake kufuatiwa na kuomba baadhi ya makampuni na mashirika misaada ambayo itaweza kuwasaidia wasichana hao kuweza kumudu hedhi zao.

Kama mwanachuo aliyemaliza lazima kuna changamoto amezipitia...

“Changamoto ya kwanza ninayokumbana nayo ni kuhusiana na jamii kutoelewa kitu gani unafanya na kwanini unafanya. Jamii yetu hususani jamii ya hijab imekua ikiona  kuzungumzia suala la hedhi salama ni kama matusi au suala la aibu sana, kitendo ambacho baadhi ya mashule wanakataa kabisa kukupa nafasi ya kuongea na wanafunzi,” amesema Shufaa Hemed.

Kama mwanafunzi ambaye tayari amemaliza chuo lazima awe na hofu na shaka ya nyinsi ya kupata kazi lakini kwa upande wa mwanadada huyo yeye anasema kuwa…

“Kazi imekua ni changamoto ambayo inamgusa kila mmoja aliyewahi kuhitimu kwa maisha ya sasa kumaliza tu chuo na kupata ajira ni ngumu inakubidi upambane utengeneze ajira yako mwenyewe (kujiajiri),” amesema Shufaa.

Akaendelea kwa kusema, “Mimi Binafsi sikuwahi peleka barua sehemu yoyote kuomba kazi ya uuguzi badala yake nafanya uuguzi kwa jamii yangu, kutoa elimu ya hedhi salama na kutumia kipaji changu cha kuongea kwa kufanya kazi na kampuni kama Afisa masoko,” amesema Binti Nassor.

Kama tunavyojua katika kila jambo mwanadamu analo ianzisha lazima atategemea kufanikiwa, kwa upande wa binti huyu yeye anaeleza kuwa “Kufuatia harakati zangu nitahakikisha hadi kufikia 2030, hedhi salama inakua ni jambo la kawaida tu nchini kwetu, Zanzibar na Tanzania kiujumla na watu ukiwaeleza kuhusiana na swala hilo hawaleti pingamizi lolote,” aliongeza.

Ambapo kwa sasa Zanzibar tumeanzisha club zinaitwa “Afya Yangu club,” lengo na madhumuni ni kuendeleza utoaji wa elimu endelevu ya hedhi salama kwa wasichana mashuleni!!

Ukiachana na harakati anazoziendesha binti huyo lakini pia anafanya kazi kama Afisa masoko (Consultant Sales and Marketing Personel) kwa ajili ya kuweza kupata fedha kidogo za kujimu na maisha.

Watu wangu wa nguvu nimewaletea binti huyo kwasababu moja tu, kuwa kitu ulichonacho kinaweza kikawa ndio sababu ya wewe kufanikiwa, so tusijidharau kabisa. Hujapata kazi sawa, amka jishughulishe na biashara au kuhudhuria event mbalimbali, ipo siku zitalipa tu.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post