Sho Madjozi akosoa bongo fleva ya sasa

Sho Madjozi akosoa bongo fleva ya sasa

Msanii wa muziki kutoka nchini Afrika Kusini, Sho Madjozi, amesema asili ya muziki wa Tanzania umepotea hivyo anatamani kuona bongo fleva ya kitambo katika usasa.

Amesema alikuja Tanzania mwaka 2008 kipindi hicho bongo fleva ilikuwa imepamba moto, Alikiba alikuwa ametoa albumu yake, ulikuwa ndiyo muda wa Cinderella, Mac muga, kidato kimoja, Anita, yaani the orijino. Anasema baada ya hapo, 2010 Diamond akaja na Mbagala.

Aidha msanii huyu amesema kabla ya Amapiano kuingia watu walianza kuchukua midundo, melodi na 'staili' za Nigeria, hadi ikafikia hatua ikawa vigumu kujua kama ni nyimbo za Kibongo kwa sababu waliiga hadi matamshi hivyo basi amesema kuchukua vitu vya watu siyo vibaya lakini angependa kuona watanzania wanakuwa na 'staili' yao wenyewe.

Sho Madjozi amefanya vizuri kwenye ngoma zake kama ‘Chale’, ‘John Cena’, ‘Huku’ na ‘Wakanda forever’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post