Sheila Mchamba, Binti anayetamani kuwa kama Tundu Lissu

Sheila Mchamba, Binti anayetamani kuwa kama Tundu Lissu

Sheila Mchamba ni mwanafunzi katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anayesomea Shahada ya Uhasibu amefunguka ndani ya Mwananchiscoop na kuweka wazi kuwa anatamani kuwa kama mwanasiasa machachari nchini, Tundu Lissu.

Mwanadada huyu ambaye amejikita katika masuala ya ujasiriamali ya mamantilie amejipambanunua kuwa anapenda mambo ya siasa na anaamini kuwa ipo siku atakuja kuwa mwanasiasa mashuhuli hapa nchini.  

“Natamani kuwa kama Tundu Antipus Lissu kwa sababu ya jitihada zake na misimamo yake ya kisiasa, kwa miaka zaidi ya ishirini mfululizo imeonekana kuwa ni ile ile. Hatetereshwi na jambo na wala hafati upepo anachokiamini yeye ndicho anachokisimamia” alisema Mchamba

Hata hivyo mbali na kupenda siasa, Sheila anafunguka na kusema kuwa yeye anajishughulisha na biashara ya mamantilie na imekuwa ikimsaidia kupata fedha za kujikimu chuoni.

Tunajua kuwa biashara hii ya mamantilie imezoeleka kuwa hufanywa haswa na watu wazima, na mabinti wengi huona aibu kufanya biashara hiyo ya mamantilie na hupendelea zaidi kuuza vitu vya urembo kama vile pochi,nguo na biashara ndogo ndogo .

Lakini kwa binti huyu yeye aliamua kujitoa muhanga na kuweka pembeni aibu na kujaribu kufanya biashara hiyo ya mamantilie.

Sheila anafanya biashara hiyo ya kuuza chakula nje ya chuo chao kipindi ambacho vyuo vimefunguliwa yaani katika muhula wa masomo (semesters).

KWANINI MAMANTILIE

Kila anayeamua kufanya biashara basi ana sababu yake muhimu inayompelekea kufanya hivyo, Sheila yeye anafunguka na kusema kuwa “Niliamua kufanya biashara hiyo kwasababu tokea mdogo nimekuwa nikitamani kuwa na pesa zangu mimi mwenyewe. Nilianza biashara mara tu baada ya kumaliza elimu yangu ya shule ya msingi.

“Hata hivyo umakini zaidi katika biashara nimeanza kuwa nao nilipofika chuo na kuamua kufungua mgahawa huo maarufu kama Mchamba Food Point,” alisema.

Sheila anasema katika kila biashara lazima kutakuwa na changamoto hivyo hata yeye amekuwa akikumbana nazo mara kwa mara ila anaweza kuzikabili na kusonga mbele kwa imani.

“Changamoto zipo japo sio nyingi sana, ila kubwa ni ile ya shughuli za biashara kusimama pindi tu vyuo vinapofungwa, hakika soko hupungua na kutokana na hali hiyo tunaamua kufunga mpaka pale vyuo vitakapofunguliwa.

“Changamoto nyingine ndogondogo ni pale unapotakiwa kulipia kila kitu kama maji, mahali pa kumwaga maji machafu, ulinzi na takataka, kwa kuyafanya hayo yote unajikuta matumizi ya pesa ni makubwa zaidi,” alisema.

Aidha Sheila alisema hajawahi kupata ugumu kuanzisha biashara hiyo licha ya baadhi ya watu kumeona kama nib inti asiyestahili kufanya kazi hiyo ya mamantilie.

“Nawashauri mabinti wenzangu wasione aibu kufanya biashara ya mamantilie kwa kuogopa kuchekwa au kusemwa vibaya, kama kazi unayoifanya inakuingizia kipato hakikisha unaifanya kwa bidii,” alisema.

Faida anayopata

Mrembo huyo alisema moja ya faida anyaoipata kutkana na bishara hiyo anayoifanya ni kupata fedha zinazomsaidia kukidhi mahitaji yake madogo madogo akiwa chuoni na nyumbani.

“Pia biashara imeniongezea heshima mimi kama binti, na nimeongeza uelewa katika mambo mengi yanayohusiana na ujasiriamali, imenisaidia kujuana na watu wengi zaidi na kushiriki mashindano yenye lengo la kuinua wasichana wajasiriamali” alisema na kuongeza

“Ushauri wangu kwa vijana wenzangu ni kwamba maisha ni kujituma. na kuweka jitihada katika kile unachokifanya, hakuna kitu kizuri kama kuwa na kipato chako mwenyewe lakini pia vitu vizuri haviji kirahisi ni kwa kufanya bidii” alisema

Haya haya mdau na mfuatiliaji wa @mwananchischoop funguka hapo chini wewe unatamani kuwa kama nani eeeeh, umejifunza nini kutoka kwa mwanadada Sheila.

Au tuambie unatamani kufanya biashara gani lakini mazingira hayakuruhusu kwa namna moja ama nyingine usiache kufuatilia magazine ya @mwananchisoop ili uweze kujifunza mbinu mbalimbali za kibiashara.






Comments 2


  • Awesome Image
    Christian lmk

    Hatare fight mamaa

  • Awesome Image
    Lulu Lyakinana

    Several times nimekua nakula chakula kwako, its yummy 🤤 good customer care 😍 kazi Nzuri pull up💪 Go girl ❤️ You got this 💕 Wish you success

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags