Shakira hana mpango wa mpenzi kwa sasa

Shakira hana mpango wa mpenzi kwa sasa

Mwanamuziki wa Colombia Shakira amefunguka kuwa hayopo tayari kuingia kwenye mahusiano rasmi badala yake anatamani kuwa na mtu wa kawaida (mchepuko).

Shakira maeyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahijiano yake na Rolling Stone kwa kueleza kwamba hayupo tayari kuingia kwenye mahusiano kwa sababu ya ustawi wa watoto wake.

Aidha alifunguka zaidi kwa kudai kuwa yeye kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine kwasasa kunaweza kuwachanganya watoto wake kisaikolojia na kihisia.

Pia msanii huyo aligusia kuhusiana na maumivu aliyoyapitia baada ya kuachana na baba watoto wake.

“Mateso niliyopitia yalikuwa makubwa zaidi ambayo sijawahi kupata katika maisha yangu yote, na yalinizuia kufanya kazi wakati mwingine. nilihisi kama mtu alikuwa amenichoma tundu kwenye kifua changu” alisema Shakira

Shakira aliachana na aliyekuwa mpenzi wake mwanasoka wa zamani Gerard Piqué mwaka 2022 baada ya kudumu kwa miaka 11 huku wakifanikiwa kupata watoto wawili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags