Shah Rukh Khan amchezesha kihindi Ed Sheeran

Shah Rukh Khan amchezesha kihindi Ed Sheeran

Wakati akiendelea na ziara yake ya kuzunguka katika mataifa mbalimbali mwanamuziki kutoka Halifax, West Yorkshire, Ed Sheeran sasa yupo nchini India na tayari amekutana na muigizaji maarufu nchini humo Shah Rukh Khan (SRK) ambapo walipata wasaa wa kuzungumza mambo kadhaa.

Ed Sheeran kupitia ukurasa wake wa Instagram ali-share video akiwa anaelekezwa jinsi ya kucheza na SRK ikiambatana na ujumbe usemao hii ni staili yetu ya kuendeleza upendo pamoja.

Aidha Ed Sheeran yuko nchini India kwa ajili ya kutumbuiza katika zaiara yake ya +-=/x (Hisabati) katika uwanja wa mbio wa Mahalaxmi mjini Mumbai Machi 16 mwkaa huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags