Shafii Dauda aiuliza TFF, Mgunda ni kocha wa timu gani

Shafii Dauda aiuliza TFF, Mgunda ni kocha wa timu gani

Ohooooo! Mambo sio mambo baada ya jana klabu ya simba kumtambulisha Juma Mgunda ambae ni kocha wa coastal union kuwa kocha mkuu wa simba kwa muda, mchambuzi na mwandishi wa michezo Shafii Dauda amewauliza swali shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kuwa kocha huyo alietambulishwa jana wanamtambua kama ni watimu gani.

Dauda kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa “Kwenye hii dunia ya weledi kuna vitu vinafanyika kienyeji na tunahitaji kuvipamba, haiko sawa na haiwezi kuwa sawa hata kidogo, TFF wanapaswa kuliweka sawa hili la Juma Mgunda, Simba na Coastal Union”

“Juma ni mwajiriwa wa Coastal Union na ana mkataba nao, kwa maelekezo ya Coastal ni kuwa bado wana mkataba nae na Simba wamesema wazi kuwa ‘wamemwazima’ kwa muda (rejea taarifa yao) mnataka kuliacha hili kuwa lipo sawa? How on earth”

“Tafsiri sahihi ni kuwa Juma Mgunda ni Kocha wa Simba na Coastal Union, yani Kocha mmoja kwa timu mbili za Ligi moja ambapo moja inacheza na Police Tanzania Jumamosi na nyingine inacheza na Nyasa kwakuwa zote zinaendeshwa kwa program zake. Hili lingewezekana endapo Juma angeenda National team kwakuwa hazina mwingilio wa kimaslahi na klabu zote, ila Simba na Coastal Union wote wana mgongano wa kimaslahi hilo halina kificho” ameandika Dauda

aidha aliendelea kwa kuandika kuwa "Kwa TFF ambao ndio wenye mpira Tanzania naomba niwaulize, Juma mnamtambua kama Kocha wa timu gani? Jibu ni Coastal Union sasa ameenda kufanya nini Simba? Na kwanini mpo kimya hamtoi ufafanuzi kama ni sahihi ama sio sahihi ijapo kiweledi jibu SIO SAHIHI, kwanini tumeamua kukaa kimya?

“Ni kweli Simba hawana Kocha Mkuu kwasasa, kama wanamtaka Juma kwa muda walipaswa kuvunja mkataba wake kwa muda ili kulinda weledi, sasa weledi upo wapi? Mbona tunataka kulichukulia jambo zito kwa njia rahisi? Ni sahihi Juma ni mzawa na tunapenda wapate nafasi kubwa kama hizi ila sasa kwa utaratibu upi?? Baada ya haya yote Coastal Union wasimame wapi na Simba wasimame wapi? Inasikitisha sana.”

“2022 nimeshuhudia Kocha mmoja anafundisha timu mbili za ligi moja, Simba ni ya Tanzania na imeenda kimataifa kupitia ligi hii ambayo Coastal Union yupo, inasikitisha sana! Wala tusiume ume maneno.FAIR COMPETITION, When DIGALA speaks, you simply listen and take note” ameandika Shafii Dauda

Huo sio walaka wangu ni wa mchambuzi mkongwe wa michezo je unanini cha kuongezea kuhusiana na hili dondosha komenti yako hapo chini .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags