Shabiki atangaza kumzawadia Mayele gari

Shabiki atangaza kumzawadia Mayele gari

Alooooooweeeh! Alooootenaah! Basi bwana kwa alichokifanya mzee wakutetema Fiston Kalala Mayele mchezaji wa yanga kuichapa Simba bao mbili katika siku ya ngao ya jamii, shabiki mmoja alijitokeza na kuahidi kuwa Yanga ikifunga atatoa Million 10 kwa kila mchezaji.

Shabiki huyo analiejulikana kwa jina la PCK, kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka na kuandika kuwa “klabu ya Yanga naomba bank account number zenu nataka kuweka pesa za wachezaji, kila mchezaji nina 10 million zake hapa, pls nataka wapewe pesa zao asubuhi na mapema wale bata,” ameandika official PCK.

Aidha aliendelea kwa kuandika kuwa “Halafu Mayele naomba afike kwenye showroom yangu iliyopo Magomeni Mikumi, achague gari yoyote anayoitaka yeye mwenyewe achukue bureeee,” ameandika PCK.



Unahisi ahadi hiyo ni ya ukweli ama ni mihemuko ya shabiki huyu tu? Tupia comment yako.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags