Shabiki amkimbiza Refa uwanjani

Shabiki amkimbiza Refa uwanjani

Muamuzi wa mchezo kati ya ‘klabu’ ya  #PortVale dhidi ya ‘klabu’ ya  #Portsmouth alijikuta akishindwa kuendelea kuchezesha mpira baada ya shabiki mmoja kuvamia uwanjani na kuanza kumkimbizi.

Mchezo huo wa ‘ligi’ daraja la pili nchini #England ulisimama kwa muda baada ya shabiki kuingia na kuanza kumkimbiza muamuzi  aliyefahamika kwa jina la Craig Hicks.

Tukio hilo lilitokea baada ya Hicks kuipa ‘penalti’ ‘klabu’ ya  Portsmouth dakika ya 88, iliyoifanya ‘timu’ hiyo kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Hata hivyo walinzi wa uwanja wakisaidiwa na ‘kocha’ wa Port Vale, #AndyCrosby walifanikiwa kumkamata na muamuzi akarejea uwanjani kuendelea na mchezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags