Shabiki achora tattoo ya kudumu kuomboleza kifo cha Mama Wizkid

Shabiki achora tattoo ya kudumu kuomboleza kifo cha Mama Wizkid

Siku chache zilizopita nyota wa muziki kutoka Nigeria Wizkid alimpoteza mama yake Mrs. Jane Dolapo Balogun, ambaye alifariki dunia Agosti 18, 2023.

Baada ya taarifa za kifo cha mama wa star huyo watu maarufu walijitokeza kutoa pole za rambirambi kwa Wizkid, akiwemo Davido , Burnaboy na wengine wengi.

Tofauti na watu hao maarufu kutoa pole, shabiki kindakindaki wa Wizkid yeye ameonesha upendo wa dhati kwa nyota huo kwa kuchora tattoo ya kudumu kwenye pajani kama kumbukumbu ya kuenzi kifo cha mama wa nyota huyo.

Katika tattoo hiyo amechora mchoro wa mshumaa huku chini yake ameandika tarehe ambayo mama wa star huyo alipoteza maisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags