Serena kuwa mcheza tenisi wa kwanza kupata tuzo ya uanamitindo

Serena kuwa mcheza tenisi wa kwanza kupata tuzo ya uanamitindo

Mchezaji maarufu wa mpira wa tenisi Serena Williams anatarajia kutunukiwa tuzo ya utambuliso wa mitindo na atakuwa mcheza tenisi wa kwanza kupewa tuzo hiyo.

Baraza la Wabunifu wa Mitindo wa Marekani (CFDA) limetoka tangazo la kumtunuku mchezaji huyo tuzo hiyo ya utambulisho wa mitindo kwa mwaka 2023 kwani amefanya mabadiliko makubwa katika ulimwengu wa mitindo kwa kuwa na mitindo ya kipekee ya uvaaji bila ya kuogopa chochote,

Thom Browne, ambaye ni Mwenyekiti wa CFDA, amesema kuwa, Serena ni mmoja wa watu wanaovutia zaidi ulimwenguni hivyo ni mfano mzuri wa mtu kuamini kile anachofanya hivyo wamemuona kuwa ni mwanamitindo halisi.

Serena Williams atatunukiwa tuzo hiyo katika hafla ya Tuzo za Mitindo za CFDA za 2023 zitakazotolewa New York Novemba 6, 2023, ambapo kutakuwa na wabunifu mbalimbali wakipokea tuzo hizo, huku Serena akiwa mchezaji pekee kwenye orodha ya wapokeaji.

Serena ni bingwa wa mara 23 wa Grand Slam na alistaafu kucheza tenisi ya kulipwa Septemba 2022, ingawa alikataa kutumia neno "kustaafu" na kutumia kupumzika, kwa sasa ameamua kutumia muda mwingi kwenye kulea watoto wake, baada ya kujifungua mtoto wa pili wa kike aitwaye Adira River Ohanian.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags