Selena Gomez sasa ni bilionea

Selena Gomez sasa ni bilionea

Mwanamuziki na mfanyabiashara Selena Gomez ametajwa kuingia katika orodha ya mabilionea ambapo utajiri wao unatokana na juhudi za kibiashara.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bloomberg imeeleza kuwa utariji huo umetokana na chapa yake ya ‘Rare Beauty’ ambapo mpaka kufikia sasa ametajwa kumiliki dola 1.3 bilioni.

Chapa ya urembo ya ‘Rare Beauty’ ilianzishwa miaka mitano iliyopita na imekuwa maarufu kutokana na kuwasaidia vijana wanaoanza kutumia vipodozi kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Tmz Selena si chapa yake tu ndiyo imemfanya kuwa bilionea kwani ameongeza utajiri wake kupitia kuanzisha kampuni ya afya ya akili ‘Wondermind’ pamoja na miradi yake ya uigizaji.

Selena Gomez anaungana na msanii Taylor Swift ambaye Aprili mwaka huu aliingia kwenye orodha ya matajiri wakubwa duniani.

Ambapo ametajwa kumiliki utajiri binafsi wa wastani wa dola 1.1 bilioni ikiwa ni sawa Sh 2.5 trilioni huku idadi hiyo ya fedha ikimfanya kuwa mtu wa 2,545 kati ya 2,781 ya mabilionea wa mwaka 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags