Selena Gomez ataja sababu kushindwa kubeba ujauzito

Selena Gomez ataja sababu kushindwa kubeba ujauzito

Mwanamuziki Selena Gomez amefunguka kuwa yupo kwenye mpango wa kuanzisha familia na mpenzi wake Benny Blanco miaka michache ijayo, lakini hatoweza kubeba ujauzito kama wanawake wengine.

Selena amefunguka hayo kwenye magazine ya Vanity Fair huku akidokeza kuwa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kupata mtoto akiwa na umri wa miaka 35

“Sijawahi kusema hili, lakini kwa bahati mbaya siwezi kubeba watoto wangu mwenyewe. Nina matatizo mengi ya kiafya ambayo yangetishia maisha yangu na ya mtoto. Hilo lilikuwa jambo lililofanya nilie kila muda,”amesema

Ikumbukwe Gomez amekumbana na matatizo mbalimbali ya kiafya hadi kupelekea apandikizwe figo lakini pia alipita kipindi kigumu cha bipolar. Na mwaka 2022 akiwa kwenye mahojiano na Rolling Stone alieleza kuwa dawa anazotumia zinaweza kumfanya ashindwe kubeba ujauzito salama.

Hata hivyo hakuacha kumzungumzia mchumba wake, pamoja na tetesi za kufunga kwao ndoa.

“Kila wakati tunajihakikishia tunalinda kile tulicho nacho, lakini hakuna sheria nataka daima awe yeye mwenyewe. Ninataka mimi pia niwe mimi mwenyewe kama tutafunga ndoa sitabadili jina langu hata kidogo. Mimi ni Selena Gomez. Hivyo ndivyo ilivyo, ”amesema

“Sijawahi kupendwa hivi Blanco amekuwa mwangaza kamili katika maisha yangu. Yeye ni rafiki yangu bora,”amesema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags