Scholes awachana mastaa Man United

Scholes awachana mastaa Man United

Mchezaji wa zamani wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited,  #PaulScholes amesema kuwa wachezaji wengi wa ‘timu’ hiyo ni wavivu na viwango vyao ni vya chini.

Ameyasema hayo baada ya ‘klabu hiyo kuruhusu bao 1-0 kwenye mchezo wao dhidi ya #Newcastle, siku ya jana.

#ManUnited ilipoteza mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa St James' Park #England, imekuwa na nyakati ngumu tangu kuanza kwa msimu huu wakiwa wamefunga ‘mechi’ sita na kushinda nane kati ya 14 za ‘Ligi’ Kuu.

“Hadi sasa hii  ndiyo ‘timu’ mbovu zaidi, matokeo yote iliyopata hivi karibuni hayakubaliki, kuna wachezaji wengi wavivu kwenye timu huwezi kufanikiwa kwa kucheza namna ile” alisema Scholes.

Kipigo hicho kiliifanya #ManUnited kuendelea kusalia nafasi ya saba ikiwa na alama 22.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags