Ikiwa ni muendelezo wa kutaja majina na vipengele mbalimbali vinavyowania tuzo za Tanzania Music Awards (TMA), sasa vimetajwa vipengele vingine ikiwemo cha Tanzania Global Icons Award (Mtanzania anayeipeperusha vema bendera ya Tanzania Kimataifa).
Katika kipengele hicho mastaa mbalimbali watatoana jasho akiwemo mchezaji wa mpira wa miguu Mbwana Samatta, mwanamitindo Flaviana Matata, wanasarakasi Ramadhan Brothers, pamoja na Anisa Mpungwe na Clara Luvanga.
Mbali na kipengele hicho kimetajwa kingine cha Best Traditional Musician of The year (Mwanamuziki Bora wa Nyimbo za Asili), wanaowania ni Elizabeth Maliganya, Erica Lulakwa, Sinaubi Zawose, Ngapi Group na Wamwiduka Band.
Aidha kipengele kingine ni Best Dance Music Song of The Year (Wimbo Bora Dansi Wa Mwaka) wanaowania ni Diamond ft Koffie Olomide na ngoma ya ‘Achii’, Melody Mbassa ‘Nyoka’, Malaika Band ‘Kanivuruga’ na Twanga Pepeta ‘Mmbea’.
Kamati ya tuzo inayoongozwa na Mwenyekiti wake David Minja na Makamu Mwenyekiti Seven Mosha imesema vipengele vingine vitaendelea kutangazwa kila baada ya muda huku zoezi la kupigia kura likifunguliwa rasmi September 3,2024.
Leave a Reply