Safari ya Yanga na Nabi imefika ukingoni

Safari ya Yanga na Nabi imefika ukingoni

Mabingwa wa nchi mara 29 Yanga Africans rasmi imetangaza kuachana na kocha wake Nasreddine Nabi ambaye amemaliza mkataba wake na kufanya uamuzi wa kutoendelea klabuni hapo.

Nyuma ya hayo ni baada ya kumalizika kwa mkataba, uongozi wa yanga ulikutana na Nabi kwa ajili ya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, lakini aliomba kuondoka ili akapate changamoto mpya.

Aidha akiwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Nabi amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi kuu, mataji mawili ya kombe la shirikisho la azam, mataji mawili ya ngao ya jamii na kuifikisha timu fainali ya kombe la shirikisho afrika mwaka huu.

Huku tetesi zikieleza kuwa kocha huyo yuko katika mazungumzo na klabu ya Kaizer chiefs ya Afrika Kusini. Haya mwanangu sana fanya kama unamtakia kheri japo roho inauma, dondosha komenti yako utueleze unamshauri nini Nabi?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags