Sababu za 50 Cent kutosimamiwa na meneja hadi leo

Sababu za 50 Cent kutosimamiwa na meneja hadi leo

Mwanamuziki wa Marekani 50 Cent ameweka wazi sababu ya kutokuwa na meneja hadi leo, huku akidai kuwa ni kheri kutoa kiasi kikubwa kwa mawakili kuliko kutoa pesa zake kwa ajili ya kumlipa meneja.

“Sina meneja, meneja anisimamie kwa nini? Wakati nakamilisha dili zangu mwenyewe mara mia ya wasanii wanaomilikiwa na mameneja, meneja hajengi chochote mimi ndiyo najenga kila kitu ni bora niwalipe mawakili tu” amesema 50 Cent

Hata hivyo aliongezea kwa kusema ameamua kusimamia kila kitu mwenyewe kuepuka makato ya asilimia ambayo kikawaida mameneja huchukua kutoka kwa msanii anayemsimamia.

Mbali na hayo amefunguka kiasi ambacho huwa anawalipa mawakili wake tangu aanze muziki kwa kudai kuwa anatumia zaidi ya dola 24 milioni ikiwa ni sawa na Sh 65.2 bilioni kwenye masuala ya kisheria ya kibinafsi na kwenye muziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags