Sababu ya kifo cha Mohbad bado ni kizungumkuti

Sababu ya kifo cha Mohbad bado ni kizungumkuti

Baada ya kusubiri majibu ya vipimo ya mwili wa mwanamuziki kutoka Nigeria Mohbad kwa miezi nane sasa, Daktari Bingwa wa Uchunguzi wa Kisayansi na Patholojia kutoka Hospitali ya Taaluma ya Chuo Kikuu cha Jimbo la Lagos (LASUTH), Prof. Shokunle Shoyemi ameleeza kuwa chanzo cha kifo cha msanii huyo hakiwezi kutambulika.

Kwa mujibu wa tovuti ya Hammer times na vyombo vya habari mbalimbali nchini humo vimeeleza kuwa Prof. Shokunle Shoyemi alitoa maelezo hayo siku ya jana Jumatato Mei 15 mbele ya Mahakama kwa kuweka wazi kuwa sababu ya kifo cha Mohbad hakikuweza kufahamika kutokana na mwili huo kufanyiwa uchunguzi ukiwa umeharibika.

Prof. Osiyemi alimweleza Hakimu Adedayo Shotobi kuwa chanzo cha kifo hakikuweza kufahamika kutokana na kuchukua takriabni siku 21 kabla ya uchunguzi wa maiti kufanyika kwa muda huo mwili ulikuwa tayari umesha haribika.

Shokunle pia alimuelezea hakimu kuhusiana na msanii kutoka na tamu baada ya kifo chake ambapo alidai kuwa madai hayo yalikuwa ni yauongo.

Mwanamuziki huyo alifariki Septemba 12, 2023 na akazikwa siku iliyofuata, kifo cha msanii huyo kilizua utata na kusababisha Serikali katika Jimbo la Lagos kufanya uchunguzi huku mwili wake ukifukuliwa kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi huo ambao ulianza Oktoba 13 mwkaa jana katika Mahakama ya Mwanzo ya Ikorodu.

Hata hivyo kesi hiyo ilihairishwa kwa siku ya jana mpaka Juni 11 mwaka huu, huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.

Kupitia kesi hiyo watu mbalimbali walikamatwa ambao walikuwa wakihusishwa na kesi hiyo moja wapo akiwa ni bosi wake wa zamani Naira Marley, Sam Larry, na rafiki yake wa karibu Primeboy, lakini watu hao walifanikiwa kutoka kwa dhamana.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post