Alooweee!! Najua mko poa wanetu wa faida nikukumbushe it’s another weekend lazima tukutane kuhabarishana mambo kadha wa kadha mtu wangu utakaaje kizembe wakati mwananchi scoop ipo kwaajili yako.
Leo katika segement yetu pendwa ya michezo na burudani tutakuwa na Isaya Michael Mtambo maarufu Chino Kiddy wengi wetu tulikuwa tukimfahamu katika maswala ya kudance.
Lakini hivi karibuni amejikita kwenye kuimba tena ameonekana kuwaka sana pale alipo wania na kupata tuzo za ‘TMA’ katika kipengele cha mwanamuzi bora wa kizazi kipya, twende kazi sasa mwanagu sana.
Mtu anapoamua kutoka nafasi nyengine kwenda nyengine hasa katika mafanikio ujue lazima kuwe na sababu zinazo kufanya utoke sehemu flani uwende kwingine kwa upande wa mwamba Chino anaeleza...
“Kilicho nisababisha niingie kwenye muziki kwanza niligundua mimi nina kipaji halafu kubwa zaidi ni kuendeleza kipaji changu cha kudance na kugundua style mbalimbali katika muziki”alisema Chino
Aliendelea kwa kusema anamshukuru Mungu alipoingia kwenye muziki watu alio wakuta katika tasinia hiyo walimpokea vizuri na kumuonyesha ushirikiano.
Licha ya kujua kucheza msanii huyo anaeleza kuwa anapotunga wimbo cha kwanza anafikiria kucheza na hapendi kufikiria vitu vyengine ambavyo vita mtoa kwenye mood ya kutunga wimbo kama mambo yanayohusu mahusiano anasema
“Sipendi kuingiza mambo ya mapenzi katika nyimbo zangu kwasababu natamani kuongelea vitu vyengine vinavyo husiana na vibe na vinavyousiana na aina nyengine ya maisha sio mahusiano sasa hivi kila mtu amekuwa akiimba nyimbo zinazohusu mapenzi”alisema Chino.
Hakuna kitu anachojivunia kama alivotafuta jina na akalipata katika muziki wake kama wanetu tunavyosema amejitafuta halafu kajipata, sasa hivi ukiambiwa leo kuna show ya Chino kid akuna mwamba anaelaza damu kwenda kujionea amekuja na kitu gani kipya anasema.
“Nilijipanga kutengeneza jina kama wasanii wengine wanavyo julikana majina yao na mitindo yao wanapo panda kwenye stage au wanapo toa nyimbo mfano Daimond, fans mwenyewe anajua hii ni ladha ya fulani kama saivi mimi unapotaja ‘Chino Wara Man’ watu wote wanajua ni nani” alisema mwanamuziki huyo.
Pamoja na hayo bhana wanasemaga hakuna tamu isiyo na chungu mwamba huu amesanuka changamoto anazozipitia kila siku katika muziki wake alio uanza hivi karibuni.
“Mtu yeyote akiwa anaanza kitu fulani haswa katika tasinia ya Sanaa ya muziki lazima apitie changamoto za kutosha tu kama kutoaminika kuwa unaweza kufanya tofauti au kwa ukubwa na watu ambao umewakuta katika tasinia husika” aliendelea kwa kueleza
“Kutokuheshimika yaani unachofikiria wewe tufauti na mwenzio anavyo kufikiria au uwezo nilio kuwa nao mimi pengine mwengine haujui. Lakini nilisha jiandaaga na hayo kabla nikapambana na naendelea kupambana naamini nitayafanikisha”alisema mwanamuziki huyo.
Pia ameweka wazi kuwa mitandao ya kijamii ndio inapush sana kazi zake kama watu kufanya challenge ya nyimbo zake kila anapo toa nyimbo mpya nakupata mashabiki wanao pendelea mtindo wake wa kuimba anasema.
“Mitandao ya kijamii imesaidia nyimbo zangu kuonekana kwa ukubwa pia napenda kuparform on stage vibe linakuwa kubwa sana napata mizuka hasa nyimbo yangu ya ‘Gibella’ inakuwaga zaidi ninapo waona fans wako on vibe na nyimbo zangu”alisema Chino.
Mbali na hayo mwamba huyo katika vitu anavyo vipenda na kuviweza kufanya mbali na muziki ana kipaji cha kucheza mpira na akitolea mfano kama utani team ya Yanga ikatokea ikampa nafasi atakimbiza hahahahaha akisema kuwa machachari yake kama ya Morrison (BM3) vile.
Wanetu sisi kama team Mwananchi Scoop tuna kila sababu ya kukwambia safari moja huwanzisha nyengine unaweza ukawa unakitu kidogo una kijua lakini ndani ya iko kidogo kuna kikubwa ukakitafuta na ukakipata.
Kama mwamba huyo alikuwa dancer tu lakini leo anatoa ngoma tena kali na jina lake kufahamika nani asiemjua Chino hivi \karibuni na machachari yake akiwa on stage.
Sasa wewe mwanetu wa faida unasubiri nini hapo sio lazima uimbe unatafuta unachokiona utakimudu na utatoboa na kufanya mambo makubwa ya msingi kwaajili ya kuielimisha jamii.
Itakuwa vizuri nikikuambia sina budi kuitupa kalamu yangu chini nitafakari next weekend nikubwagie nini katika burudani mwanangu sana.
Leave a Reply