Sababu ya Apple kubadili mfumo wa ‘chaji’

Sababu ya Apple kubadili mfumo wa ‘chaji’

Baada ya kampuni ya Apple kuzindua toleo jipya la Iphone 15 na kueleza kuwa simu hiyo haitatumia tena ‘chaji’ iliyozoeleka katika simu hizo na baada yake Iphone hiyo itatumia USB-C, jambo ambalo limewashangaza wengi huku baadhi ya watumiaji wakitafsiri kuwa kampuni hiyo huwenda imefirisika ndiyo maana wakashindwa kutengeneza ‘chaji’ iliyozoeleka.

Sasa basi jambo ambalo wengi  hawafahamu kuhusiana na kampuni hiyo ya teknolojia imethibitisha kuwa simu za iPhone mpya hazitatumia ‘kebo’ yake iliyozoeleka katika kuchaji simu baada ya mfumo wa chaji kubadilishwa kufuatia sheria zilizowekwa na Umoja wa Ulaya (EU).

Umoja wa Ulaya iliiambia kampuni hiyo kuachana na ‘kebo’ inazotumia ili kurahisisha maisha kwa watumiaji, kuokoa pesa, na kusaidia kupunguza taka za kielektroniki, pia vifaa vyote vinavyobebeka kuendana na ‘chaja’ inayotumika kuchaji simu za aina zote ulimwenguni ifikapo Desemba 2024.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags