Sababu School Bus kuwa na rangi ya njano

Sababu School Bus kuwa na rangi ya njano

Si jambo la kushangaza kama ukitembelea mataifa mbalimbali na kukuta magari ya kubebea wanafunzi (School Bus) yakawa na rangi ya kufanana, yaani rangi ya njano. Fahamu kuwa rangi hiyo kwenye mabasi ya shule iliidhinishwa April mwaka 1939 na mtaalamu wa elimu aliyefahamika kwa jina Frank W. Cyr.

Sababu kubwa ikiwa njano inaonekana kwa urahisi zaidi gizani na hii ndiyo moja ya sababu kuu kuchaguliwa kutumiwa kwenye magari ya shule, huku lengo likiwa kulinda usalama wa wanafunzi usiku au mchana kwa kuonekana haraka zaidi na kuepusha ajali.

Sababu ya pili kuwekwa kwa rangi ya chano na maandishi meusi ni kufuatiwa na giza la asubuhi hivyo rangi hiyo na maandishi yake itamsaidia mwanafunzi kuona basi hilo kwa haraka zaidi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags