Saba wajeruhiwa baada ya lift kudondoka

Saba wajeruhiwa baada ya lift kudondoka

Watu saba wamejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Kairuki kwa ajili ya matibabu baada ya lifti kuporomoka kutoka ghorofa ya 10 katika jengo la Millenium Tower lililopo Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Jeshi la zimamoto na uokoaji limesema chanzo ni lifti hiyo iliyokuwa imebeba zaidi ya watu kumi kuzidiwa uzito ilikuwa imefanyiwa matengenezo hivi karibuni ambapo leo ilikuwa inajaribiwa.

Askari wa zimamoto na uokoaji Inspekta Msaidizi Mohammed kutoka Kinondoni amesema kilichofanywa na uongozi wa jengo hilo lenye ghorofa 25 ni makosa kwa kuwa hawakupaswa kufanya majaribio ya lift kukiwa na watu ndani bali walitakiwa kuweka kitu chochote chenye uzito ili kukamilisha marekebisho hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags