Ryerson yaanzisha kozi ya Drake, Theweeknd

Ryerson yaanzisha kozi ya Drake, Theweeknd

Chuo cha Ryerson kilichopo Toronto Canada kimeanzisha kozi za mastaa wa muziki kutoka nchini humo ambae ni Aubrey Drake maarufu kama Drake na Abel Makkonen maarufu kama Theweeknd, itakayo anza rasmi 2022.

Kupitia kozi hiyo ya Drake na Theweeknd wanafunzi wataweza kujifunza kuhusu rekodi mbalimbali zilizowekwa na mastaa hao pamoja na safari yao ya kimuziki.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Professa wa chuo hicho Daltone Higgins ambapo alieleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo sio chuo hicho tu kinachotoa kozi za mastaa na wanamuziki, kutoka nchini Marekani kuna kozi ya JayZ katika chuo cha George Town University na Beyonce kozi katika chuo cha Texas University.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags