Rwanda yaishutumu Kongo kwa kumfukuza balozi wake

Rwanda yaishutumu Kongo kwa kumfukuza balozi wake

Rwanda imemshutumu jirani yake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuchochea wasiwasi baina yao baada ya Kongo hapo jana kumuagiza balozi wa Rwanda kuondoka nchini humo katika kipindi cha masaa 48.

Imeelezwa, hatua hiyo inafuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya uasi mashariki mwa Kongo, wakati taifa hilo likiamini kwamba Rwanda inawasaidia waasi wa M23 wanaozidi kujiimarisha kwenye eneo hilo tangu mwaka uliopita.

Kwenye taarifa yake, baada ya balozi Vincent Karega kufukuzwa, Rwanda imesema inasikitishwa kuona Kongo inaendelea kuifanya Rwanda kama mbuzi wa kafara, ili kuficha na kuvuruga udhaifu wake kiutawala na kuongeza kuwa vikosi vyake vilivyoko mpakani vinasalia katika tahadhari.

 Kundi la M23 limekuwa kiini cha mvutano baina ya mataifa hayo mawili, na usiku wa jana Umoja wa Afrika ulisema una wasiwasi mkubwa kutokana na kutetereka kwa hali ya usalama katika eneo hilo la mashariki mwa Kongo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags