Ruger: Naweza kupenda wanawake watano kwa wakati mmoja

Ruger: Naweza kupenda wanawake watano kwa wakati mmoja

Mwanamuziki wa Nigeria, Ruger amefunguka mtazamo wake kuhusu mahusiano  kwa kudai kuwa anaweza kupenda wanawake watano tofauti kwa wakati mmoja.

 Ruger ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mahojiano na ‘The Beat FM’ na kueleza kuwa  hana desturi ya huangukia kwenye upendo kirahisi, huku akisisitiza kuwa pongezi humfanya awe na hisia kwa wanawake.

 “Ninaweza kupenda wanawake watano tofauti kwa wakati mmoja, sijui kama inawezekana kwa wengine lakini naweza kuifanya na kwa kweli nitawapenda.

"Ni rahisi kwangu kupenda kwa maana zawadi na pongezi hunifanya niwe na hisia kwa wanawake kwa sababu ninathamini sana zawadi na pongezi” alisema.

Hata hivyo msanii huyo hakuishia hapo pia amefafanua kuwa licha ya kufanya majaribio ya aina nyingine katika upande wa muziki hawezi kuacha kuimba Afrobeats kwa sababu ndiyo inampatia mahusiano mazuri na mashabiki zake.

Ruger mwenye umri wa miaka 24 amewahi kufanya ngoma zilizompatia umaarufu ndani na nje ya Nigeria, nyimbo hizo ni kama ‘Asiwaju’, ‘WeWe’, Bounce, Poe, Dior, Snapchat, ‘Girlfriend’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags