Rude Boy awaonya wazazi wanaoshauri watoto wao kutafuta masponsa

Rude Boy awaonya wazazi wanaoshauri watoto wao kutafuta masponsa

Mwanamuziki nchini Nigeria Rude Boy, ametoa ushauri kwa wazazi mwenye watoto wa kike wanaoamini kuwa mwanaume ndiye mwenye jukumu la kughalamikia maisha ya mabinti wakati wote.

Kupitia Instastory ya Rude amewataka wazazi kuacha kuwalazimisha watoto wao wa kike kuomba fedha kwa wanaume kwani suala hilo limesababisha wasichana wengi kudanganywa huku wengine kuathiriwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya Legit imeeleza kuwa ushauri alioutoa Rude ni baada ya kuwepo kwa matukio kadhaa kwa mabinti kudhurika kutokana na kujirahisisha.

Ushauri huo huenda ukaendana na takwimu mpya za hivi karibuni zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) zikionesha ongezeko kubwa la maambukizi ya VVU kwa wasichana waliozaliwa miaka ya 2000.

Huku sababu kubwa ikiwa kujirahisisha, mahusiano baina ya mabinti hao na watu wazima pamoja na matumizi mabaya ya teknolojia.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post