Rubani afariki kwa ajali baada ya kufichua jinsia ya mtoto

Rubani afariki kwa ajali baada ya kufichua jinsia ya mtoto

Imekuwa kawaida siku za hivi karibuni wazazi watarajiwa kutumia mbinu mbalimbali kutambulisha jinsia ya mtoto wanaye mtarajia kwa kutumia rangi ya blue hutambulisha mtoto wa kiume na pink hutambulisha wa kike, hivyo basi hutumia mbinu za kibunifu kuweka rangi hizo.

Kupitia sherehe ya kufichua jinsia ya mtoto iliyofanyika Sinaloa, Mexico, imegeuka kuwa huzuni baada rubani wa ndege ambayo ilikuwa maalumu kwa kuweka wazi jinsia ya mtoto wa wanandoa kufariki dunia kwa ajali baada ya kufichua jinsia.

Rubani huyo aliyefahamika kwa jina la Luis Angel N, alipitisha ndege na kumwaga rangi ya pink katika sherehe hiyo kwa maana ya kuwa mtoto mtarajiwa  ni wakike, lakini baada ya kufanya tukio hilo ndege ilibadilisha muelekeo na kubinuka kisha idondoka chini na kusababisha kifo chake.

Inaelezwa kuwa wakati huo familia haikuweza kugundua ajali hiyo waliendelea na sherehe kwani ndege ilipitiliza na kwenda kupindukia mbele, lakini baada ya muda kidogo ndipo walipata taarifa ya ajali hiyo iliyopelekea sherehe yao kugeuka huzuni.

Tukio hilo limepelekea baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutoa ushauri wa watu kuangalia namna bora ya kushangilia ujio wa watoto wao na sio kufanya vitu vya kuhatarisha maisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags