ROMA: Wakitoa hit utasikia nilikaa kimya kwa muda mrefu

ROMA: Wakitoa hit utasikia nilikaa kimya kwa muda mrefu

 Msanii wa muziki wa #HipHop nchini Roma Mkatoliki, ametupa jiwe gizani kwa baadhi ya wasanii wenye tabia ya kudai walikaa kimya kwa muda mrefu, mara baada ya kuona wametoa ngoma na ikafanya vizuri.

 Roma ameandika hayo baada ya kuona baadhi ya wasanii, wakidai kurudi rasmi kwenye muziki baada ya kimya cha muda mrefu. Kupitia ukurasa wake wa #Tweeter Roma ameandika,

“Unakuta Msanii Anatoa Ngoma Kila Leo, Sema Tu Zinakataa Zinakuwa Either Hazifanyi Vizuri Saaanaaa Au Kawaida Tu Hazipokelewi Kwa Ukubwa Huuoo!! Then Inatokea Hapo Hapo Anaotea  Anaachia Ngoma Moja  Na Inaenda Ina Hit Raia Wanaipokea Kwa Ukubwa……

UTASKIA ANASEMA NILIKAA KIMYA MUDA MREFU SANA😁 WENGINE WANATAJA HADI MIAKA (MINNE) GAME ILIKUWA IMEPOA SANA😁SASA NDIO NIMEANZA RASMI!!

Yani Zile Zilizokuwa Zinakataa Kataa Anakuwa Kama Anajizima Kifurushi Hivi Hazi-Count…..Anasingizia Alikuwa kimya!

Game Haijawahi Kupoa…..Wana Kibao Wamekichafua Toka January Huko….

Au Mnataka Kusema Club Kuanzia January Walikuwa Wanapigaga Gospel , Qaswida? Au Zilipendwa?”

Unahisi jiwe la Roma analitupa kwa nani?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags