Roma: sihusiki kwenye wimbo wa Nay, namba zake za simu sina

Roma: sihusiki kwenye wimbo wa Nay, namba zake za simu sina

Baada ya msanii Nay wa Mitego kudai kuwa mistari ya wimbo wa amkeni ambao kwa sasa umefungiwa kuna baadhi ya mistari ametumiwa na #Roma, sasa roma amejibuka na kukanusha madai hayo.

Madai hayo ya Nay kuandikiwa mistari aliyatoa kwenye  #Interviw aliyofanyiwa na  moja ya chombo cha habari nchini,  #Mkatoliki ameshindwa kuvumilia na kushusha walaka kupitia ukurasa wake wa twitter na kudai kuwa hausiki na mistari ya wimbo huo na wala hana namba za simu za Nay.

Roma ameandika,

“#YAH: SIHUSIKI KWENYE HILI.

Kwenu #BasataTanzania Husika Na Kichwa Cha Habari Hapo Juu, Huyu Kijana NAY  Ni Muongo Sana, Mimi Sijamtumia Kitu Chochote Wala Sijahusika Kwenye Wimbo Wake Huo, Kwanza Hata Namba Yake Ya Simu Sina, Ananisingizia Na Sijapenda!! Mimi Ni Kijana Muadilifu Sana NA MNALIJUA HILO #BasataTanzania

Naipenda Sana Nchi Yangu, Zidumu Fikra Za Mwenyekiti  Na Kazi Iendelee……!!

#NB Akija Hiyo Jumatatu, Malizaneni Naye PekeYake, Mimi Nina Familia Na Watoto Wananitegemea Kupitia Mziki, Sitaki HekaHeka!!”

#MwananchiScoop

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post