Roboti Muhammad azua gumzo mitandaoni

Roboti Muhammad azua gumzo mitandaoni

‘Roboti’ wa kwanza wa kiume kuzinduliwa nchini Saudi Arabia aitwaye Muhammad azua gumzo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kumpapasa ripota wa kike wa runinga ya ‘Saudi Arabia Al Arabiya’ jambo ambalo lilitafsiriwa vibaya na wadau mbalimbali nchini humo.

‘Roboti’ hiyo wa kwanza wa kiume alizinduliwa katika mkutano wa ‘teknolojia’ mjini Riyadh mwanzoni mwa mwezi Machi, ambapo lilitengenezwa na kampuni ya ‘QSS Systems’.

Aidha kupitia mtandao wa X (zamani twitter) kulizuka mijadala mbalimbali huku baadhi ya watu wakidai kuwa kitendo hicho ni unyanyasaji kwa ripota huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags