Robo fainali ya Simba ipo hapa

Robo fainali ya Simba ipo hapa

Baada ya ‘klabu’ ya Simba kupoteza point mbele ya ‘klabu’ ya #WydadCasablanca jana nchini Morocco kwa bao 1-0, sasa ‘klabu hiyo inahitaji kushinda ‘mechi’ zake mbili za hapa nyumbani kufufua matumaini ya kucheza robo fainali ya ‘Ligi’ ya Mabingwa msimu huu.

Simba imebakiwa na ‘mechi’ tatu, hadi sasa imekusanya alama mbili tu, kwenye ‘mechi’ tatu ilizocheza ikiwa ndiyo inaburuza mkia kwenye kundi B.

‘Mechi’ zake mbili za nyumbani ya kwanza itakuwa ni dhidi ya Wydad na Jwaneng Galaxy ambazo ikishinda itakuwa imefikisha alama nane huku ikiziombea Wydad na Jwaneng zifanye vibaya kwa kutoa sare.

Mbali ya ‘mechi’ dhidi ya Jwaneng na Wydad, mchezo mwingine ni ule wa ugenini dhidi ya Asec Mimosa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags