Robertinho awekwa kikaangoni, Kipigo cha Yanga

Robertinho awekwa kikaangoni, Kipigo cha Yanga

Kocha mkuu wa ‘Klabu’ ya Simba Roberto Oliveira 'Robertinho' anatajwa kukalia kuti kavu kutokana na matokeo ya ‘mechi’ iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam amabapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Inaripotiwa kuwa baada ya mchezo huo, viongozi wenye ushawishi ndani ya Simba wakiwemo wale ambao awali walikuwa wanamuunga mkono Robertinho, wanaonekana kupoteza imani naye na wanatoa ushauri kuwa 'kocha' huyo awekwe kando.

“Kuhusu uamuzi wa kumtimua bado haujafanywa na wala hatujakaa kuzungumzia hilo kama inavyoandikwa mitandaoni. Tumeona tuwe watulivu kwa sasa ili tusifanye uamuzi wa presha lakini kiuhalisia nafasi ya kocha kubakia ni finyu,” amesema mmoja wa viongozi wa Simba.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags