Robertinho awakalia kooni wachezaji wake dhidi ya ‘mechi’ ya marudiano na Dynamos

Robertinho awakalia kooni wachezaji wake dhidi ya ‘mechi’ ya marudiano na Dynamos

Akiwa katika kikao na wachezaji wake ‘kocha’ wa ‘Klabu’ ya #Simba, #Robertinho amesema kuwa kuna mkataba muhimu wamekubaliana na ‘timu’ yake kuwa wataingia na akili kubwa kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya #PowerDynamos wakiwa na lengo moja tu kuthibitisha ubora wa kikosi hicho.

Aidha inadaiwa kukubaliana yeye na ‘timu’ yake kwamba makosa yaliyozalisha sare ya mabao 2-2 ugenini, nchini #Zambia hayakuwa ya mtu mmoja au wawili ni ya ‘timu’ nzima ilikosea, lakini dakika 90 za nyumbani zitakuwa na mabadiliko makubwa.

Hakuacha kuweka msisitizo kwa wachezaji wake akiwataka wakati wanajiandaa kucheza na #CoastalUnion akili zao ziwaze kulinda heshima kwa kuhakikisha kikosi chao kinatinga kibabe makundi ya #CAF.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags