Robertinho akosoa usajili Simba

Robertinho akosoa usajili Simba

Aliyekuwa ‘Kocha’ wa #Simba #Robertinho amekosoa usajili uliofanywa na ‘klabu’ hiyo kwa kueleza kuwa usajili uliofanywa katika dirisha kubwa haukuwa na tija kutokana na kundi kubwa la wachezaji kutokuwa na ubora.         

#Robertinho alisema kuwa kati ya wachezaji 11 waliosajiliwa na ‘timu’ hiyo katika dirisha lililopita, ni wawili tu ambao wameonekana kuweza kushindania nafasi katika kikosi cha kwanza ambao ni beki Che Fondoh Malone na kiungo #FabriceNgoma. 

"Hakuna njia ya mkato kwenye kutafuta mafanikio kupata timu Bora huwezi kuijenga kwa kutumia dirisha moja la usajili, sikiliza kwenye usajili uliopita tuliwaleta wachezaji wengi lakini ni wawili tu wanaweza kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza. 

Wachezaji 11 waliosajiliwa na Simba katika dirisha lililopita  ni Ngoma, Malone, Hussein Kazi, Ayoub Lakred, Aubin Kramo, Luis Miquissone, Shaban Chilunda, Hussein Abel, David Kameta, Willy Onana na Hamisi Abdallah.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags