Rihanna aonesha ujauzito wake mwingine

Rihanna aonesha ujauzito wake mwingine

Mwanamuziki maarufu kutoka Barbados Rihanna inasemekana kuwa anaujauzito mwingine na hii imejulikana katika show aliotumbuiza ya Super Bowl 2023 iliofanyika katika uwanja wa Arizona’s.

Kupitia jarida la Rilling Stone limethibitisha kuwa mwanamuziki huyo na mpenzi wake Asaprocky wanatarajia kumkaribisha mgeni mwingine katika familia yao.

Katika mahojiano yake wiki iliyopita, Rihanna aliulizwa kama kutakuwa na suprize wakati wa onyesho lake kwenye Uwanja Arizona's State Farm Arizona.

“Nafikiria kumleta mtu, mwimbaji lakini Sina uhakika, tutaona siku ,hiyo ikifika” alisema Rihanna

Kwa kawaida mashabiki walidhani kwamba alikuwa akizungumza kuhusu mmoja wa wasanii wengi ambao alishirikiana nao wakati wa kazi yake ya sanaa.

Lakini Rihanna hakuwa akimaanisha yeyote kati yao na alikuwa akidokeza kwamba alikuwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Ndani ya saa moja baada ya onyesho la Rihanna kufikia tamati, huku mashabiki wake wakijadiliana kuhusu muda gani ujauzito wake umedumu wawakilishi wake walithibitisha kuwa mwimbaji huyo alikuwa na ujauzito wa mtoto wake wa pili.

Ingawa baadhi ya mashabiki walikiri kusikitishwa na kwamba hii itamaanisha kuchelewa tena kwa albamu ya tisa ya Rihanna.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags