Rihanna anatarajia kupata mtoto wa tatu

Rihanna anatarajia kupata mtoto wa tatu


Baada ya kuzua taharuki kufuatia ‘tisheti’ yake iliyoandikwa nimestaafu, sasa imeripotiwa kuwa mwanamuziki Rihanna anatarajia kupata mtoto wa tatu na mpenzi wake A$AP Rocky.

Taarifa ya Rihanna kutarajia kupata mtoto wa tatu inakuja baada ya video kusambaa kupitia mitandao ya kijamii ikimuonesha akiwa anaficha tumbo na mkoba wake wakati alipokuwa matembezi jijini New York na mpenzi wake Asap.

Ikumbukwe kuwa siku tatu zilizopita Riri alikatisha mitaa ya New York akiwa amevalia ‘tisheti’ iliyoandikwa ‘I AM RETIRED’ ikiwa na maana amestaafu jambo ambalo limewakatisha tamaa mashabiki wengi kusubiri albumu mpya kutoka kwa mwanamuziki huyo huku mara ya mwisho kuachia album ikiwa ni 2016.

A$AP Rocky na Rihanna walianza uhusiano wao rasmi mwaka 2020 na kubahatika kupata watoto wawili ambao ni RZA na Riot.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags