Rema apokelewa kwa kishindo kwao

Rema apokelewa kwa kishindo kwao

Waswahili wanasema nabii hakubaliki kwao lakini msemo huu umekuwa tofauti kwa mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Rema ambaye amepokelewa kwa kishindo nyumbani kwao katika kijiji alichozaliwa cha Benin, jimbo la Edo, Nigeria.

Mapema jana Rema alitua kijijini kwao na kupokelewa kwa shangwe ambapo amefika katika ardhi hiyo alipozaliwa kwa ajili ya show yake inayotarajiwa kufanyika Ijumaa hii Agosti 30 katika Uwanja wa Samuel Ogbemudia.

Lebo inayomsimamia msanii huyo ya Mavin, ilishiriki video ya kuwasili kwake kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) ikiandika “Benin, mwana wako maarufu Mkuu wa Afrobeats Rema yuko Nyumbani!"

Utakumbuka kuwa tamasha hilo lilitangazwa kwa mara ya kwanza na mwimbaji wa Ozeba Julai mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags