Rekodi alizoweka SZA kupitia albamu yake SOS

Rekodi alizoweka SZA kupitia albamu yake SOS

Leo Desemba 9 album ya SZA inayoitwa 'SOS' imetimiza miaka 2 tangu kuachiwa kwake huku, mkali huyo akitangaza kuachia toleo jipya la album hiyo ya SOS (Deluxe) hivi karibuni.

Hizi ni baadhi ya rekodi ambazo album ya SOS imeweka kwa SZA

1,Ilishika namba moja kwenye Billboard Hot 200

2,Ilikuwa albamu ya kwanza ya SZA iliyouza copy 318K ndani ya wiki yake ya kwanza kutoka.

3,Ilikaa namba moja kwenye Billboard 200 kwa wiki 10 mfululizo.

4, Ilipata streams zaidi ya milioni 405 kwenye wiki yake ya kwanza kutoka.

5, ‘SOS’ ilikaa wiki 21 kwenye chati za juu za albamu za R&B/Hip-Hop rekodi hizi ni ndefu zaidi kuwahi kutokea kwa msanii wa kike.

6, RIAA iliipatia albumu hiyo platinum certificate mara tatu mwaka 2023.

7, Wimbo wa 'Snooze' kutoka kwenye albumu hiyo ulishinda Wimbo Bora wa R&B kwenye tuzo za GRAMMYS 2023, huku ‘SOS’ ikitwaa tuzo ya Best Progressive Albamu huku akiwa na jumla ya ushindi wa GRAMMY nne tangua aanze muziki.

Katika chapisho la SZA hivi karibuni kupitia kwenye Insta story yake aliweka picha ya cover iliyotumika kwenye album ya SOS huku neno 'Deluxe' likiwa limeandikwa juu na baadhi ya majina ya nyimbo yakiwa yamefutwa huku wimbo pekee ambao umeachwa ni SATURN wimbo ambao ulitoka Februari 24 mwaka huu.

Ikumbukwe mwezi uliopita SZA aliweka wazi mpango wake wa kutoa albamu mbili, 'SOS Deluxe Album' na 'LANA' ambayo inatarajiwa kuwa albumu yake ya tatu itakayotoka kabla ya Tour yake na Kendrick Lamar itakayoanza Mei 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags