Refa matatani kwa kumchoma kisu mchezaji

Refa matatani kwa kumchoma kisu mchezaji

Muamuzi wa mpira wa miguu anayefahamika kwa jina la #RemigioArmoa atuhumiwa kumchoma kisu mchezaji wa ‘timu’ ya #Chacarita, #Kevin, baada ya kuzuka vurugu kati ya wachezaji kwenye ‘mechi’ ya madaraja ya chini Argentina.

Tukio hilo lilitokea katika mji wa Scholler katika jimbo la Misiones, nchini humo, Video iliwaonesha wachezaji wakimsukuma refa ambaye baada ya kuona amezidiwa alichomoa kisu na kumchoma mchezaji kifuani.

Baada ya tukio hilo refa alikimbia eneo hilo, huku mchezaji huyo akionekana kudondoka chini na baadhi ya watu wakijaribu kumpa msaada wa kumtoa nje ya uwanja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags