RC Mtaka : Walimu wapya uhamisho marufuku

RC Mtaka : Walimu wapya uhamisho marufuku

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewaonya Walimu wa ajira mpya wenye matarajio ya kuomba uhamisho wa vituo vya kazi mara baada ya kupata ajira kuacha tabia hiyo mara moja.

Mtaka ametoa kauli hiyo kufuatia kitendo cha Watumishi wengi kuwa na tabia ya kuomba uhamisho mara baada ya kuona changamoto kwenye maeneo yao ya kazi.

Aidha Mtaka ametoa onyo hilo katika kikao cha uzinduzi wa vitabu vya mwongozo wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mkoa alipokutana na Walimu wapya wa Mkoa huo katika Shule ya Sekondari Mpechi iliyopo Mjini Njombe.

“Ni lazima muangalie nyuma kwa shukrani na mjue kuna Maelfu ya wenye degree za elimu wamekosa kazi, sitarajii kuona Mtu anahangaishana na Afisa Elimu kumwambia naomba nihamishie kituo fulani na Afisa Elimu usibebe dhambi ukiona simu yeyote mwambie nendeni kwa Mkuu wa Mkoa, kama hautaki acha kazi uende kwenu” amesema Anthony Mtaka

Dondosha koment yako hapo chini mwanangu sana je alichokisema muheshimiwa ni sahihi au laaaah!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags