Rayvanny awatolea povu wanaodai anapita na upepo

Rayvanny awatolea povu wanaodai anapita na upepo

Baada ya kuzuka tetesi kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na mwanamuziki wa #Bongofleva #Rayvanny kwenda na upepo wa kufanya ‘kolabo’ na wasanii wanao-hit, #VannyBoy amekanusha tetesi hizo kwa kueleza kuwa akifanya ngoma na msanii yoyote basi ameamua kufanya haendi na upepo kama watu wanavyo fikiria.

Kupitia ukurasa wa Instagram amewajia juu wote wanaozungumzia suala hila kwa kueleza kuwa kama angetaka kufanya ‘kolabo’ na nyimbo zilizohit basi angefanya wimbo wa ‘Enjoy’ au ‘Single Again’ ambazo alitumiwa beat kabla.

“Msifanye nianze kukataa kufanya nyimbo na vijana wenzangu wakiniomba kufanya kazi”

Ikumbukwe kuwa Rayvann ameshafanya ‘kolabo’ mbili na wasanii chipukizi ambao ngoma zao zina-hit kupitia mitandao ya kijamii akiwemo Miso Misondo na Dayoo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags