Rayvanny aupigia promo muziki wa singeli, Uingereza

Rayvanny aupigia promo muziki wa singeli, Uingereza

Mwanamuziki wa #Bongofleva nchini Rayvanny akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake katika nchi mbalimbali ameanza kuupigia debe muziki wa Singeli, huku akitaka ulimwengu kuskiliza muziki huo kutokana na kuwa na vibe.

Rayvanny ameyasema hayo wakati alipokuwa katika mahojiano yake na Podcast ya ‘The 3Shotsoftequila’ ambapo alieeleza kuwa ni wakati wa Dunia sasa kuskiliza sound tofauti licha ya kuwepo muziki wa #Afrobeat lakini upo muziki wa Singeli ambao asili yake ni Tanzania na unavibe sana.

Aidha pia alipata wasaha wa kumzungumzia Dj Miso Misondo pamoja na wazee wa Makoti walivyoweza ku-trend kupitia mtandao wa Tiktok, ambao aliwatafuta na kufanya nao kazi.

Miso pamoja na Rayvanny walifanikiwa kutoa ‘kolabo’ ya ngoma iitwayo ‘Kitu Kizito’ ikiwa na zaidi ya watazamaji milioni 3 kupitia mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags