Rayvanny aumia plan yake kutofanikiwa

Rayvanny aumia plan yake kutofanikiwa

Mwanamuziki anayedaiwa kusifika kuwa na ubunifu mkubwa akiwa jukwaani #Rayvanny kwa masikitiko makubwa aliyokuwa nayo kupoteza show aliyokuwa anataka kuonyesha Mbeya kwa kupata hasara ya maandalizi ya show hiyo ilio mgharimu millioni70 kwaajili ya maandalizi hayo.

Katika ukurasa wake wa #Instagram ame-post video iliokuwa ikionyesha eneo ambalo ililokuw likitengenezwa mfano wa bahari ilionyeshe uhalisia wakutumbuza akiwa ndani ya boat lakini eneo hilo kabla ya show iliharibika na kupata hasara.

Rayvanny ameandika ujumbe kuwa hiyo show ingefanyika ingekuwa ni moja ya show ya ndoto yake kuwahi kutokea na ni show ambayo alikuwa anaisubiri Kwa muda mrefu kufanaya.

Aidha amekiri kutumia gharama kubwa ilimradi lengo lake litime, japo alifanya umakini katika matengenezo hayo ya show ila mpango wake wote haukufanikiwa na kuingiwa na huzuni, ila anasema kuwa ni mipango ya Mungu kuwa hivyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags