Raya: Sijaja kwenye maisha ya Barnaba kwa bahati mbaya

Raya: Sijaja kwenye maisha ya Barnaba kwa bahati mbaya

Raya ambaye ni mke wa mwanamuziki Barnaba Classic kupitia mahojiano yake na moja ya chombo cha habari amefunguka na kueleza kuwa hakuingia kwenye maisha ya barnaba kwa kukurupuka kama wasemavyo watu.

ameyasema hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na watu wanavyo izungumzia ndoa yake kwa kudai kuwa bidada huyo amelazimisha kuolewa na #Barnaba. Raya amesema,

“Kwanza Barnaba kunioa sijaja kwenye maisha yake kwa bahati mbaya tulipitia changamoto nyingi sana, alivyoachana na mama watoto wake nilipambana nae sana, mwaka 2016-17 nikaanza nae akiwa hana chochote nataka watu wafahamu

“Nime-hustle na mwanaume wangu tumeanzia chini, Barnaba amekuja kwangu akiwa hana chochote yaani nimeanza nae akiwa hana chochote vyote aliacha kwa mama watoto wake, vitu vyote unavyomuona yuko navyo sasa hivi ni ameanza na mimi, tumeanza moja nilipitia wakati mgumu sana kwa sababu mwenzangu alishazoea maisha ya familia kwa hiyo alikuwa na strees nyingi sana, lakini nikajitahidi kama mwanamke nilisimama kama mwanamke mpaka leo vile mnavyo muona”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags