Ratiba ya Kanye kuja Afrika imekuwa tofauti

Ratiba ya Kanye kuja Afrika imekuwa tofauti

Baada ya kutangaza kurudi tena Africa kwa ajili ya kusikiliza album yake iitwayo ‘Velturels’, uongozi wa mwanamuziki Kanye West umetoa taarifa nyingine ikieleza kuwa tukio hilo limesitishwa mpaka pale watakapo tangaza tena.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mwanamuziki huyo wametoa taarifa hiyo kwa kuwaomba radhi mashabiki ambao wamenunua tiketi kwa ajili ya eventi hiyo huku wakiwaahidi kutangaza tarehe nyingine siku za hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa Kanye ambaye kwa sasa anatamba na albumu ya ‘Vultures’ alipanga kuja Africa kwa ajili ya usikilizaji wa albumu yake kwenye Pyramid za Saqqara nchini Misri, Aprili 20, 2024.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Kanye kutua Africa, mara ya mwisho ilikuwa 2018 ambapo alitua Uganda kwa ajili ya kumalizia albumu yake ya ‘Yandhi’ ambayo bado haijatoka mpaka sasa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags