Rashford, Mwanamitindo Erica wadaiwa kuwa wapenzi

Rashford, Mwanamitindo Erica wadaiwa kuwa wapenzi

Imedaiwa kuwa mchezaji wa klabu ya Manchester United, Marcus Rashford ameingia katika mahusiano na mwanamitindo kutoka nchini Colombia, Erica Correa baada ya hivi karibuni kuonekana wakiwa pamoja katika kumbi za starehe.

Kwa mujibu wa The Sun News imeeleza kuwa wawili hao wamekuwa gumzo mitandaoni ambapo baadhi ya watu wana hisi huwenda wakawa katika mahusiano ya kimapenzi.

Rashford mwenye umri wa mika 26 alionekana akiwa na mwanamitindo huyo mzaliwa wa Colombia kwenye ukumbu wa starehe katika jiji la Manchester nchini Ungereza siku ya Jumapili jioni.

Inadaiwa kuwa nyota huyo wa Man United tangu alipoachana na mpenzi wake Lucia Loi  mwaka 2023 hakuwahi kuonekana na mwanamke kwa ukaribu hivyo kama alivyo kuwa na mwanamitindo huyo.

Rashford na Lucia Loi walianza kuwa katika mahusiano miaka nane iliyopita wakiwa na umri wa miaka 15 wakiti wapo shule ya Aston iliyopo Manchester na kuachana mwaka 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags