Rashford aonesha jeuri ya pesa baada ya kupata ajali

Rashford aonesha jeuri ya pesa baada ya kupata ajali

‘Staa’ wa Manchester United Marcus Rashford baada kupata ajali akiwa anaendesha gari yake aina ya Rolls-Royce Wraith yenye thamani ya Pauni 700,000(Tsh 2.1 bilioni), aonekana tena kwenye ndinga nyingine mpya aina ya ‘Mercedes van’ aliyoinunua siku chache zilizopita kwa Pauni 180,000(Tsh 549 milioni).

Rashford mwenye umri wa miaka 25, alionekana kwenye gari hiyo mpya akiwasili kwenye viwanja vya mazoezi vya Carrington lakini alikuwa akiendeshwa.

Gari hiyo mpya ndani yake ina ‘gemu’, sehemu za kuchajia  na eneo kubwa ambalo linamuwezesha kulala ikiwa atahitaji,‘Staa’ huyu wa kimataifa wa England alipata ajali jumamosi ya week iliyopita wakati anarudi nyumbani kwake baada ya mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Burnley lakini hakuumia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post