Rapcha aangaliwe kwa jicho la tatu

Rapcha aangaliwe kwa jicho la tatu

Kwenye muziki wa #HipHop kwa bongo wasanii ni wengi na kila mmoja huwa na aina ya uandishi wake kwenye upande wa mistari, wapo wale wazee wa ‘disi’, na wale wa ngumu kumeza.

Kwa upande wa mwanamuziki wa HipHop Rapcha, amekuwa na utofauti mkubwa sana katika ngoma zake hasa upande wa uandishi, kama wewe ni mfuatiliaji wa muziki wake utakuwa unaelewa kinacho maanishwa hapa.

Mara nyingi msanii huyu amekuwa mtu wa kuandika mistari ambayo imekaa katika mtindo wa masimulizi, na wakati mwingine huwa anatoa muendelezo kama inavyokuwa kwenye movie.

Uzuri ni kwamba Rapcha hajaanza au kuishia kwenye Lissa tu kuhusu aina hiyo ya uandishi, amekuwa hivyo tangu kipindi cha Unaua Vibe akiwa na #Mbuzi Lunya , na sasa tunaona akiendelea na mtindo huo kwenye ngoma zake kama vile, #Hello, #Uongo na nyingine nyingi.

Ukijaribu kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, utagundua kuwa mashabiki wengi wanapenda uandishi wa aina anayofanya huku wapo wale wanao- comment kwa kudai kuwa #Rapcha aangaliwe kwa jicho la tatu kwenye upande wa Movie kwani anaweza kuwa mzuri zaidi upande huo.

Unaukubali wimbo gani wa mkali huyo?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags